Posts

Image
  Na John Mapepele Waziri Wa Utamaduni, Sanaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amehimiza umuhimu wa kumuenzi mwanaharakati  mwanamke, Bibi Titi Mohamed aliyefanya kazi kwa karibuni na Mwalimu Julisu Nyerere katika harakati za kuleta uhuru wa Tanganyika. Akizungumzia tamasha  la Bibi Titi Mohamed litakalofanyika  wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, Mhe. Mchengerwa kwenye kipindi cha 360 cha kituo cha televisheni cha Clouds leo ambapo amesema  Bibi Titi ni alama ya mabadiliko katika suala zima la ushiriki wa wanakwake katika harakati hizo na kuleta mabadiliko.  “Ukimzungumzia Bibi Titi Mohamed unazungumzia alama ya mabadiliko, unazungumia alama ya kutoka kutoamini kuja katika kuamini kwa sababu Bibi Titi  mwenyewe aliamini kwamba tunaweza kujikomboa,” amesema. Amesema ni vigumu kuzungumzia mabadiliko ya kisiasa ya kuwaingiza wanawake katika siasa, ushawishi wa katika siasa, uchumi, matumizi ya Kiswahili,  bila kumzungumzia Bibi Titi Mohamed.   Amesema...

Mhe. Mhengerwa -Tamasha la Sanaa Bagamoyo ni la kimataifa, Makamu wa Rais afafanua kuwa Sanaa inaongoza katika ukuaji wa uchumi nchini

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema  Serikali imefanya  maboresho makubwa   kwenye Tamasha la mwaka huu la 41 la Utamaduni na Sanaa   Bagamoyo kuwa la kimataifa ambapo limeshirikisha nchi mbalimbali duniani ili kuitangaza Tanzania na utamaduni wake duniani. Kauli hiyo ameitoa leo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais Mhe, Dkt. Philipo Mpango kuzindua rasmi tamasha hili kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano. Mhe. Samia  Suluhu Hassan. Ameongeza kuwa tamasha hili limeshirikisha vikundi vya wasanii kutoa mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Canada, Zambia, Burundi na Visiwa vya Mayote kutoka nchini Ufaransa. “Mwaka huu tumeendelea  kuliboresha Zaidi tamasha hili kutoka kuwa tamasha la mazoea la wanafunzi wa sanaa hapa chuoni ili kulipatia hadhi zaidi ya kuwa tamasha la kimataifa.” Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha amesema wameteleza maelekezo ya Mhe. Rais ya kutaka kuendeleza tamasha hili n...

Mhe. Kikwete aipongeza Wizara kwa kukuza Sekta ya Sanaa kwa kasi, adai ina mchango mkubwa kwenye uchumi

Waziri Mchengerwa atoa siku 30 kwa BMT kutengeneza mifumo ya kusajili ya kielektoniki

Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakiksha ndani ya mwezi mmoja linatengeneza mfumo wa kieletroniki wa kusajili vyama vya michezo ili kuondoa usumbufu kwa wadau unaojitokeza. Mhe. Mchengerwa ameyasema  haya  leo Oktoba 27, 2022 wakati akizindua program ya “Mpira Fursa” inayoratibiwa na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO) na kugawa  vifaa vya michezo kwa  Vyuo vya Wananchi vya  Maendeleo 54 kote nchini na shule za msingi 86.   Ameutaka uongozo wa shule ambazo zitabahatika kupata vifaa vya soka, kuwaruhusu wasichana kucheza soka na kuvitumia vifaa hivyo kwa uangalifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.   Ameipongeza KTO kwa kuanzisha program hiyo ya kupeleka  michezo  katika vyuo vya  wananchi  vya maendeleo na shule za msingi huku akifafanua kuwa  huo ni utekelezaji wa  maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza...

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 16, 2022 amezindua  zoezi la  kitaifa la  kuibua na kusaka vipaji  vya Sanaa la "Mtaa kwa Mtaa" eneo la  Ikwiriri wilayani Rufiji, zoezi ambalo litafanyika nchi nzima. Akizindua zoezi hilo katika eneo la Ikwiriri, Mhe. Mchengerwa amesema eneo linalofuata baada ya uzinduzi wa leo ni Mkoa wa Arusha ambapo litafanyika kila mtaa ili kuibua vipaji kwenye sanaa. Amewataka watanzania  wenye vipaji vya Sanaa kujitokeza wakati wa zoezi hilo likiendelea  ili waweze kuendelezwa baada ya kuibuliwa, huku akisisitiza  kauli ya Kipaji chako ndiyo mtaji wako. "Ndugu zangu hii ni ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu, Rais anatamani kuona misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ya kuthamini na kuendeleza Sanaa inaendelezwa ili kuwanufaisha vijana" amesisitiza,  Mhe. Mchengerwa   Amezitaka mamlaka za wilaya na mikoa kote nchini kusai...

MCHENGERWA AITAKA COSOTA KUTOA ELIMU YA KANUNI MPYA ZA ADA ZA VIBEBEA KAZI ZA SANAA NA MAKAMPUNI YA WASANII

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA)  kutoa elimu ya kutosha kwa wadau hususan wabunge      kuhusu mabadiliko makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo ya kimuundo na kisekta ili kusaidia kuinua maisha ya wadau wa sekta ya Sanaa nchini. Waziri Mchengerwa ameyasema haya leo Septemba 14, mara baada ya kupitishwa  yeye na Naibu wake Mhe, Pauline Gekul na Menejimenti ya taasisi hiyo kwenye kikao cha kujadili  rasimu ya kanuni ya uanzishwaji wa Ada kwa vibebea kazi za ubunifu (blank device) na uanzishwaji wa makampuni binafsi ya   wasanii ya ukusanyaji na ugawaji mirahaba (CMO). Amewataka kuharakisha mchakato wa kukamilisha rasimu hizo ili  zisainiwe  na kuanza kutumika mara moja hatimaye wasani na wadau mbalimbali wa kazi za Sanaa waweze kunufaika na kazi zao. "Harakisheni, ninakwenda kuisaini kanuni hizi mara moja ili wasanii  wafaidi matunda ya...

KUPOKEA TAARIFA YA KUSIMAMIA HAKIMILIKI NA UGAWAJI WA MIRAHABA NA MASHUJAA WA JUMUIYA YA MADOLA

Image
                       Na Mwandishi wetu– Dodoma  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa kesho Agosti 12, 2022, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kupokea  taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Ugawaji wa  Mirahaba kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa ya Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzia saa 11 jioni jijini Dar es Salaam.  Uteuzi wa Kamati hiyo, ulitokana na malalamiko ya wadau hususan wa Sekta ya  Sanaa nchini kuhusiana na namna mirabaha inavyokusanywa na kugawanywa,  kuwepo kwa vitendo vya uharamia katika kazi zao na elimu duni kwa wadau  kuhusu masuala hayo.  Aidha, uundaji wa Kamati hiyo ulitokana na maelekezo ya Mhe. Rais ya  kuitaka Wizara kusimamia na kutafuta muarobaini wa changamoto za  mirabaha kwa wasanii aliyoitoa Mei 30, 2022 jijini Dar es ...